H Baba ajiweka shakani kwa Harmonize

Mwaka jana/juzi H Baba alijitoa kwenye uwanafamilia wa Konde Gang ya Harmonize na kuhamia Wasafi family ya Diamond Platnumz, baada ya kuondoka kwa Harmonize alitoa maneno mengi machafu na udhalilishaji huku akimsifia Diamond Platnumz kwa kumuomba msamaha na kumsujudia miguuni.

Baada ya mambo kwenda ndivyo sivyo tofauti na matarajio yake, familia ya Diamond imekuwa ikionyesha kutokuwa na muda nae, kumnyima upenyo wa kula chungu kimoja.

H Baba ameamua kurejea kwenye kambi yake ya awali ya Konde Gang na bila hiyana Harmonize amempokea kwa mikono miwili baada ya kumpigia magoti na kujutia maamuzi yake ya kuisaliti kambi ya Konde Gang.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI