Coastal Union yarudisha fedha za Lawi, Simba SC
Klabu ya Coastal Union ya Tanga imerudisha fedha ambazo Simba SC walikuwa wamelipa kwaajili ya uhamisho wa beki wa kati Lameck Lawi.
Coastal wamethibitisha kufuta dili hilo wakidai Simba imekiuka makubaliano ambayo yapo kinyume na utaratibu.
Jana kupitia mitandao iliweka wazi usajili wa Lawi katika klabu ya Simba lakini baadaye Coastal wakapinga vikali usajili huo