Clatous Chama aitosa Simba na kusaini Yanga

Na Ikram Khamees

Kiungo mshambuliaji wa Wekundu wa Msimbazi, Clatous Chama raia wa Zambia amegoma kuongeza mkataba kwenye klabu yake na tayari imefahamika kwamba muda wowote anatambulishwa Yanga SC.

Habari zenye uhakika kabisa tena bila shaka yoyote zinasema kwamba Chama amekubali kutua Yanga kwa kandarasi ya mwaka mmoja wenye mshahara wa milioni 20 na ada ya usajili milioni 200.

Chama amekataa kusaini Simba, kwani hakufurahishwa kabisa na sakata lake lilitokea mwishoni mwa msimu uliopita, Chama anadai anataka kucheza na Khalid Aucho, Stephanie Aziz Ki na Prince Dube.

Kwa maana hiyo Yanga itakuwa moto wa kuotea mbali kutokana na majina ya wachezaji hao yalivyokuwa makubwa


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI