Che Fondoh Malone ataka kuondoka Simba
Beki wa kati Che Fondoh Malone ameanzisha mtifuano akifosi aondoke ikidaiwa kuwa hana furaha ndani ya Simba SC, utata umeongezeka baada ya Future ya Misri kuonyesha nia ya kumtaka beki huyo aliyejiunga na Simba msimu uliyopita.
Viongozi hawataki kumuuza kwani inshu ya Henock Inonga imekaa vibaya, hivyo kuruhusu kuondoka kwa miamba hii miwili itapelekea safu ya ulinzi ya Simba SC kuwa wazi jambo ambalo Klabu hawakujiandaa nalo.