Augustine Okrah apewa thank you Yanga
Ni rasmi, Augustine Okrah hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao.
Baadhi ya viongozi wa Yanga SC walitaka Okrah abaki lakini kocha Miguel Gamondi amewaambia kuwa, Okrah hayupo kwenye mipango yake, Yanga ichague kati ya Gamondi na Okrah, nani abaki !.
Okrah amevunjiwa mkataba rasmi, amerejea katika klabu aliyotoka, Bechem United.
Okrah na wanasheria wake wamesema wataipeleka Yanga SC (FIFA) ikiwa hawatawalipa pesa wanazodai.