Alikamwe akiri Yanga kudaiwa na FIFA ila sasa safi

“Ni kweli tulikuwa na tunadaiwa na Mamadou Doumbia, Lazarus Kambole lakini tulikuwa kati kati ya msimu tukaona tujikite kwenye vipaumbele vilivyopo vya klabu kumaliza msimu vizuri na kuchukua makombe, jambo ambalo tumefanikiwa” Ali Kamwe Meneja wa Habari na Mawasiliano Yanga Sc.

“Baada ya msimu kukamilika tuka ‘clear’ madeni yote tuliyokuwa tunadaiwa. Kabla ya Dirisha la usajili kufunguliwa sisi Yanga tulikuwa tumeshafanya malipo yote kwa 100% ya hawa wachezaji wawili.”

“Juni 14, 2024 tulituma Proof Of Payment FIFA na Jana, Juni 18 tulipokea Email kutoka FIFA kwamba wamejiridhisha na malipo yetu.”

“Kwa taarifa rasmi ni kwamba hakuna kesi yoyote FIFA inayohusisha Young Africans, jambo la Okrah muda ukifika litakuja kuzungumzwa kulingana na ripoti ya mwalimu mwenyewe kama atabaki au ataondoka,” — Ali Kamwe kupitia Wasafi FM.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI