ZUCHU ADAI HARMONIZE AMEBAKIA KUCHAMBANA TU
Mwimbaji wa Bongofleva, Zuchu amemtolewa uvivu Harmonize na kusema alichobakiza ni vichambo tu!.
Kauli ya Zuchu inakuja baada ya Harmonize kuonekana kukejeli malalamiko ya mrembo huyo dhidi ya Diamond Platnumz.
"Harmonize huna hit mjini, una kazi ya kuchambana tu...." ameandika Zuchu katika Insta Story na kuongeza.
"Baba mzima kazi kudandia visivyokuhusu, mwanamke wako yupo busy kuomba nafasi kwa huyo anayejifanya nusu yako shenzi" - Zuchu.