YANGA NA MASHUJAA KESHO MTOTO HATUMWI DUKANI

Na Ikram Khamees. Kigoma

Kesho ndio kesho katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara inayodhamimiwa na benki ya NBC, Yanga SC watakapokuwa uwanjani dhidi ya wenyeji wao Mashujaa FC.

Mchezo huo unatazamwa kuwa mkali na wa upinzani hasa kwakuwa kila timu inamahitaji yake, Yanga inayoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 62 na inahitaji kushinda ili itangaze ubingwa mapema jambo ambalo litakuwa gumu kwa Mashujaa kuiona Yanga ikitwaa ubingwa mikononi kwao.

Mashujaa nao wapo nafasi mbaya kwani sasa wanashika nafasi ya 14 wakiwa na pointi 23 hivyo wanataka kushinda ili wafikishe pointi 26 ambazo zitawashusha Geita Gold na Ihefu.

Jioni ya leo Yanga wamefanya mazoezi kabambe kujiandaa na mchezo huo wa kesho


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI