GUEDE AENDELEA KUCHEKA NA NYAVU
Yanga SC imeendelea kuchanja mbuga baada ya jioni ya leo kuilaza Mashujaa FC bao 1-0 katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma mchezo wa Ligi Kuu bara.
Kwa ushindi huo Yanga inazidi kuongoza ligi ikiwa na alama 65 ikisaliwa mechi. 4 kukamilisha Ligi hiyo huku Mashujaa ikiwa kwenye hali mbaya.
Bao pekee la Yanga limefungwa na Joseph Guede dakika ya 41 huku akiwa na mwendelezo mzuri wa kucheka na nyavu
𝗚𝗨𝗘𝗗𝗘 𝗢𝗡 𝗙𝗜𝗥𝗘
Katika michezo (5) ya mwisho ya Yanga ligi kuu yenye sawa na points (15) ambapo Yanga wamepata points (13), Joseph Guede amechangia points (12)
Na anafunga magoli muhimu tu
Mechi (6) za mwisho alizocheza Guede :
◉ vs Singida Fountain Gate — ⚽⚽
◉ vs Simba Sports Club — ⚽
◉ vs JKT - Aligongesha mwamba
◉ vs Coastal Union — ⚽
◉ vs Tabora United (FA) — ⚽
◉ vs Mashujaa FC — ⚽'