Adam Adam avunja mkataba Mashujaa
Klabu ya Mashujaa FC yenye maskani yake mkoani Kigoma imeachana na mchezaji wake Adam omary Adam baada ya kufikia makubaliano baina ya pande zote mbili.
Adam alijiunga na Mashujaa mwanzoni mwa msimu huu akitokea Ihefu yenye maskani yake Mkoani Mbeya lakini kwa sasa ni Mkoani Singida.
Amehusika katika magoli 9,amefunga 7 na kutoa pasi za usaidizi wa mabao 2.