CAF YAMKUMBUKA MBWANA SAMATTA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemkumbuka nahodha wa kikosi cha timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbwana Samatta @samagoal77 kwa kuchapisha picha yake katika ukurasa rasmi wa CAF.

Picha ya Samatta anayekipiga PAOK ya nchini Ugiriki imewekwa katika ukurasa huo na kuandikia maneno mfungaji mabao, mnyanyua mataji na muweka historia.

Ndani ya Afrika nyota huyo aling’aa na klabu ya TP Mazembe ya nchini Congo na amewahi kushinda nayo mataji mbalimbali ya Afrika na makombe ya ndani.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI