BALAMA MAPINDUZI ATUA COASTAL UNION
Timu ya Coastal Union imekamilisha usajili wa winga wa zamani wa klabu za Alliance,Yanga na Mtibwa Sugar Balama Mapinduzi kwa mkataba wa miaka miwili.
Mapinduzi aling' ara na kikosi cha Yanga lakini aliumia katika mchezo kati ya Yanga na Simba na akakosekana kwa muda mrefu, huenda atarejesha makali yake akiwa Coastal inayonolewa na Mwinyi Zahera