SIMBA KUANGUKIA KOMBE LA SHIRIKISHO KAMA AZAM IKICHUKUA KOMBE LA FA KESHO
"Kama Bingwa wa ligi kuu akiwa bingwa wa kombe la shirikisho yule mshindi wa pili kwenye ligi kuu ataenda kuiwakilisha nchi klabu bingwa.
Kama bingwa wa Azam sports federation cup atakua yule ambae sio bingwa wa ligi kuu basi yeye ataenda klabu bingwa akiungana na bingwa wa ligi kuu.
Katika mchezo wa kesho ikiwa Azam Fc atakua bingwa wa FA basi Simba Sc na Singida Big Stars ndio ambao wataenda shirikisho.
Kama Yanga atachukua kombe hili pia basi Simba Sc ataenda klabu bingwa huku Singida Big Stars na Azam FC wao wakienda Caf confederation cup.
Sio mimi ni kanuni tu ambayo imeeleza katika kwenye Sura ya 3, kanuni ya 8 inayoelezea mshindi na uwakilishi kimataifa