JULIUS MWAKATIKA: ALIKUWQ MSHAMBULIAJI HATARI WA SIGARA, ALIITESA YANGA MIAKA YA 90

MIAKA ya mwishoni mwa 1980 na mwanzoni mwa 1990 jina la Julius Mwakatika lilitokea kuwa gumzo kwenye medani ya mchezo wa soka. 

Julius Mwakatika alikuwa miongoni mwa mchezaji mahiri wa timu ya Sigara FC ya Chang' ombe wilayani Temeke ambayo ilikuwa inamilikiwa na kiwanda cha kutengeneza Sigara kinachofahamika kama TCC Company Limited. 

Timu ya Sigara ilikuwa miongoni mwa timu zinazoshiriki Ligi daraja la kwanza Tanzania bara ambayo kwa sasa inajulikana kama Ligi Kuu bara, Sigara ilitokea kuwa timu tishio na kiboko ya vigogo.

Mwakatika hatowasahau Samuel Owu, Kasa Musa,Abeid Kasabalala, kacheza nao akiwa Sifa Politan ya Mtoni, mwaka 80 alijiunga na timu ya Wonder Boys ya daraja la pili, mwaka 82 alijiunga Sigara ikiwa daraja la pili.

 Sigara ilikuwa inanolewa na Badi Saleh akudumu misimu miwili ikiwa daraja la pili na kisha akaenda Bora FC mwaka 1987 alirudi tena  Sigara na akaisaidia timu hiyo kupanda Ligi daraja la kwanza.

Wakati huo timu hiyo ilikuwa na wachezaji kama Abubakar Salum, Edgar Fongo, Gregoly Luanda, Nathan Chamlomo, Peter Lucas, Maarufu Yassin, Hamisi Kondo, Muscat Said na wengineo.

Mwakatika aliwahi kuzifunga Simba na Yanga na anakumbuka aliwahi kumtunhua kipa wa Simba Mackenzie Ramadhan. 
Yanga mara tatu na alikuwa mwiba mkubwa kwa Yanga, anakumbuka aliifunga Yanga katika ushindi wa mabao 3-0 katika uwanja wa Taifa, sasa Uhuru jijini Dar es Salaam. 

Katika ushindi huo magazeti kama Uhuru linalomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi liliandika Sigara yaifunga ndembendembe, Mwakatika alikuwa mshambuliaji na anakumbukwa kwa kufanya mambo mengi ikiwemo kuwasaidia wachezaji wengi kucheza mpira kwenye timu za Ligi daraja la kwanza.

Mmoja wa wachezaji aliowasaidia ni Kasongo Athuman. Mwakatika alisifika kwa ufungaji na aliwahi kuwa mfungaji bora wa timu, hatosahau pale alipoachwa kwa figisu akidaiwa ni mkubwa na ikabidi wasajiliwe wengine.



Mwakatika aliibukia timu ya Messina ya Magomeni kota jijini Dar es Salaam pale zilipojengwa ghorofa mpya za kota, mchezaji huyo alikuwa mahiri uwanjani kiasi kwamba alipendwa na kila mtu hasa kwa timu za mchangani kabla ya kusajiliwa na timu kubwa. 

Mwakatika alizaliwa mkoani Mbeya mwaka 1962 na jijini Dar es Salaam alikuja baada ya wazazi wake kuhamia ambapo alibahatika kusoma shule ya msingi Magomeni.

Mwakatika alijaaliwa umbo zuri la kimichezo kwani alikuwa na nguvu ya kupambana na mabeki walioshiba na wababe, ikumbukwe timu ya Sigara ilisifika kwa kucheza soka la kibabe, na.

Pia Mwakatika alikuwa na ball control, anajua kupiga chenga za maudhi na kumtoka adui yake kwani alikuwa mjanja mno, Mwakatika alikuwa na uwezo wa kupiga mashuti makali na makipa wengi walimuogopa sana. 

Mshambuliaji huyo alikuwa na uwezo wa kutoa pasi maridadi na pia alikuwa na uwezo wa kufunga kwa vichwa au mguu, ingawa hajawahi kuitwa timu ya taifa, lakini alikuwa na uwezo mkubwa.



Mwakatika anaitaja timu ya Messina Linea kama daraja kwake lililomfikisha hapo, kwani alicheza na vijana waliokuwa na vipaji ambapo hakusita kuwataja baadhi kama Abdul Mashine na Issa Athuman

Alamsiki


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI