Metacha Mnata aongeza miwili Yanga
Kipa Metacha Mnata ameongeza mkataba wa miaka miwili katika klabu ya Yanga, lakini hatua hiyo imemtolea dirishani kipa Erick Johola aliyekuwa na siti ya kudumu benchi na jukwaani.
.
Metacha alijiunga na Young Africans Sports Club kwa mkopo wa miezi sita katika dirisha dogo la usajili la msimu huu akitokea Singida Big Stars (SBS) unaomalizika mwishoni mwa msimu huu.