YANGA YATINGA ROBO FAINALI FA CUP
Na Mwandishi Wetu. Songea
Klabu bingwa ya soka Tanzania bara, Yanga Sc jioni ya leo imefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup baada ya kuilaza Majimaji ya Songea mabao 2-1 uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.
Yanga walijipatia bao la kuongoza lililofungwa na kiungo mshambuliaji Pius Buswita kunako dakika ya 40, hadi mapumziko walikuwa mbele kwa bao hilo, kipindi cha pili Majimaji nao walicharuka wakitaka kusawazisha.
Lakini ukuta wa Yanga ulikuwa imara, dakika ya 57 Yanga walipata bao la pili lililofungwa na Emmanuel Martin aliyepokea pasi ya Hassan Kessy, vijana wa Majimaji walijipatia bao la kufutia machozi likifungwa na Jaffari Mohamed.
Nayo Mtibwa Sugar imeungana na Yanga kucheza robo fainali baada ya kuilaza Buseresere ya Geita mabao 3-0 uwanja wa Nyamagana, Mwanza, michuano hiyo itaendelea tena kesho Kiluvya United ikiwakaribisha Prisons uwanja wa Filbert Bayi mjini Kibaha, na Stand United ikiwaalika Dodoma Fc