Yanga yatinga raundi ya kwanza Ligi ya mabingwa Afrika
Na Paskal Beatus. Victoria
Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga Sc jioni ya leo imefanikiwa kuingia raundi ya kwanza ya michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kulazimishwa sare na wenyeji Saint Louis ya Shelisheli ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Linite mjini Victoria.
Timu zote zilishambuliana kwa zamu kipindi cha kwanza na Yanga wakafanikiwa kujipatia bao la kwanza lililofungwa na Ibrahim Ajibu aliyepokea pasi ya Hassan Kessy dakika ya 45.
Hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele, kipindi cha pili wenyeji Saint Louis walijaribu kulifikia lango la Yanga na kufanikiwa kusawazisha kupitia kwa Betrand Esther