Yanga vitani kesho na Majimaji
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga Sc kesho Jumatano wataikaribisha Majimaji Fc mchezo wa Ligi Kuu Bara uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Yanga inayokamata nafasi ya pili ikiwa na pointi 34 ikiachwa nyuma kwa pointi saba na mahasimu wao Simba Sc ambao wana pointi 41 wanatazamiwa kufanya vema zaidi ili kuikaribia Simba ambayo yenyewe itashuka uwanjani keshokutwa Alhamis.
Simba itakuwa ugenini Shinyanga itakapowafuata Mwadui Fc katika uwanja wa Mwadui Complex, awali mechi hizo ilikuwa zichezwe mwishoni mwa wiki lakini kutokana na vilabu hivyo viwili kukabiliwa na mechi za kimataifa, Bodi ya Ligi ikaamua kuzirejesha nyuma mechi hizo hadi Jumatano na Alhamis