YANGA KUTUPA KARATA YAKE YA KWANZA KIMATAIFA LEO

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga Sc jioni ya leo wanaanza kampeni yao ya kushiriki Ligi ya mabingwa barani Afrika itakapowakaribisha mabingwa wa Shelisheli, Saint Louis mchezo wa Raundi ya awali, uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Wawakilishi hao wa Tanzania wataingia uwanjani wakiwa na matumaini tele hasa baada ya kurejea kwa baadhi ya wachezaji wake waliokuwa nje wakiuguza majeraha yao.

Kwa bahati nzuri kipa tegemeo Mcameroon, Youthe Rostand atarejea langoni baada ya kukosekana, Rostand aliumia katika mchezo dhidi ya Ihefu Fc, mbali na Rostand, nyota wake wengine Ibrahim Ajibu, Juma Abdul, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe na Andrew Vincent waliungana na wenzao kujiandaa na mchezo huo wa leo.

Mabingwa hao wa Bara wamekuwa na matokeo mazuri kwenye mechi zao za ndani hivyo inawapa matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo huo na itawategemea zaidi nyota wake Papy Kabamba Tshishimbi, Pius Buswita na Obrey Chirwa ambao wanaunda kombinesheni hatari inayoitwa TBC

Yanga inatupa karata yake ya kwanza kimataifa leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA