Wachezaji Majimaji wagoma kucheza na Yanga kesho

Nawandishi Wetu. Dar es Salaam

Wachezaji wa kikosi cha kwanza cha timu ya Majimaji Fc ya Songea wamegoma kuichezea timu hiyo hadi kuhatarisha uwepo wao kesho wakati timu yao itakapoumana na Yanga Sc mchezo wa kombe la Azam Sports Federation Cup hatua ya 16 bora katika uwanja wa Majimaji.

Kocha wa Majimaji Habibu Kondo ameingia mchecheto jana mazoezini baada ya wachezaji wake wote wa kikosi cha kwanza kugomea mazoezi wakishinikiza kulipwa fedha zao za usajili na mishahara.

Kondo ilibidi awajumuhishe wachezaji wa kikosi cha pili wapatao 14 ili kesho Jumapili waweze kuivaa Yanga ambayo tayari imeshawasili Songea leo na ndege, lakini mwenyekiti wa timu hiyo, Steven Ngonyani amesema kwa sasa suala lao wamelipeleka kwa mbunge wao Damas Ndumbaro na mambo yatakuwa safi

Majimaji Fc wamegoma kucheza na Yanga kesho

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA