Tshishimbi aing' arisha Yanga, ikiipiga 4G Majimaji

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga Sc jioni ya leo imeendelea kutakata baada ya kuichapa Majimaji ya Songea mabao 4-1 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Ushindi huo moja kwa moja unaifanya Yanga ifikishe pointi 37 sasa ikiwa nyuma ya pointi nne na mahasimu wao Simba Sc wanaokamata usukani wa Ligi hiyo wakiwa na pointi 41 lakini wana mechi moja mkononi.

Furaha ya Wanayanga ilianzia dakika ya 18 ilipoandika bao la kwanza lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na kiungo wake Mkongoman, Papy Kabamba Tahishimbi kabla ya Mzambia Obrey Chirwa kufunga bao la pili dakika ya 29.

Yanga waliongeza bao la tatu dakika ya 43 lililofungwa kwa shuti kali na winga, Emmanuel Martin, hadi mapumziko Wanajangwani hao walikuwa mbele kwa mabao hayo, kipindi cha pili kilianza kwa kasi lakini Majimaji waliokuwa pungufu baada ya beki wake Mwakanjuki kutolewa kwa kadi nyekundu nao walipata penalti dakika ya 56 iliyowapa bao la kwanza lililofungwa na Marcel Boniventure.

Yanga walihitimisha kalamu ya mabao kunako dakika ya 83 goli likifungwa tena na Mkongoman Papy Kabamba Tshishimbi, Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa mchezo mmoja ambapo Mwadui Fc wataialika Simba uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.

Yanga imeidunga Majimaji 4-1 leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA