Township Rollers yaifuata Yanga Ligi ya mabingwa Afrika
Hatimaye sasa klabu bingwa ya Tanzania Bara, Yanga Sc itaumana na timu ya Township Rollers ya Botswana katika michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika.
Yanga jana imevuka raundi ya kwanza kwa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Saint Louis ya Shelisheli ambapo jana walitoka nayo sare ya 1-1 katika uwanja wa Linite mjini Victoria.
Lakini wawakilishi wa Botswana, Township Rollers wao walifanikiwa kuvuka raundi ya kwanza baada ya kupita kwa jumla ya mabao 4-2 hasa baada ya jana kufungwa na wenyeji El Marreikh ya Sudan mabao 2-1, mchezo wa kwanza Township Rollers ilishinda mabao 3-0 nyumbani