Tenga, Mwenyekiti mpya BMT
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Waziri wa Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni, Mhe Harrison Mwakyembe amemteua Leodegar Chila Tenga kuwa mwenyekiti mpya wa Baraza la Michezo la Taifa, (BMT) akimrithi Dioniz Malinzi aliyefutwa kazi.
Tenga amewahi kuhudumu kama Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini, (TFF) ataanza majukumu hayo kuanzia sasa na pia ana kazi kubwa kuhakikisha michezo nchini inapiga hatua.
Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa, Taifa Stars iliyobahatika kufuzu kwa mara ya kwanza fainali za mataifa Afrika zilizofanyika Lagos Nigeria mwaka 1980, pia amewahi kuzichezea Yanga Sc na Pan Africans