Stand United yaizamisha Singida United

Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam

Timu ya Stand United ya mkoani Shinyanga, jana imeifunga Singida United bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uwanja wa Namfua mkoani Singida.

Huo ni mwendelezo mzuri kwa Stand United ambao wameanza kujiondoa taratibu katika janga la kushuka daraja lakini pia yamekuwa matokeo mabaya kwa Singida United inayonolewa na Mholanzi Hans Van der Pluijm katika vita ya kuwania ubingwa wa bara.

Endapo Singida United ingeibuka na ushindi katika mchezo huo ingepaa hadi nafasi ya pili kwakufikisha pointi 36, sasa inabaki katika nafasi yake ya nne ikiwa na pointi 33 wakati Stand iliyokuwa nafasi ya 12 na pointi zake 16 sasa inakwea hadi nafasi ya 8 ikiwa na pointi 19 sawa na Mbao Fc ambao nao wametoka sare tasa 0-0 na Mtibwa Sugar uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Matokeo mengine, Njombe Mji Fc ililazimishwa sare tasa na Mbeya City uwanja wa Sabasaba Njombe, na kikosi cha Ruvu Shooting kikaikandika Lipuli Fc ya Iringa mabao 3-1 uwanja wa Mabatini, Mlandizi Pwani, leo hii Kagera Sugar wanaikaribisha Azam Fc uwanja wa Kaitaba, Bukoba

Kwa habari kamili gonga www.mambouwanjani.

Stand United wakishangilia ushindi 

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA