Singida United yaipigisha kwata Polisi Tanzania, lakini yapata pigo
Na Alex Jonathan. Dar es Salaam
Timu ya Singida United imefanikiwa kuingia robo fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuipigisha kwata timu ya Polisi Tanzania kwa mabao 2-0 katika uwanja wa Namfua mjini Shinyanga.
Ushindi huo wa leo moja kwa moja unawafanya waungane na Njombe Mji ya Njombe ambayo nayo iliwaondosha mashindanoni Mbao Fc kwa mikwaju ya penalti 6-5 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.
Katika mchezo wa leo hadi mapumziko timu hizo mbili zilikuwa bila bila, Singida United walijipatia mabao yao kipindi cha pili kupitia kwa beki wake Kennedy Wilson dakika ya 70 na Mzimbabwe Tafadzwa Kutinyu dakika ya 77.
Wakati huo huo uongozi wa Singida United unatoa salamu za pole kwa mchezaji wake Nizar Khalfan kwa kufiwa na mama yake mzazi