Simba yaitandika Gendarmarie 4-0 mbele ya mzee Ruksa

Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Simba Sc jioni ya leo imeichakaza bila huruma timu ya Gendarmarie ya Djibout mabao 4-0 mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Ikicheza mbele ya mgeni wa heshima, Rais mstaafu wa awamu ya pili mzee Ally Hassan Mwinyi, Simba ilianza kuwainua vitini mashabiki wake waliojitokeza kuishuhudia, goli likifungwa dakika ya kwanza na Said Ndemla.

Furaha ya mabao iliendelea tena katika dakika ya 33, nahodha John Bocco "Adebayor" aliipatia bao la pili kabla tena dakika ya 45 kufunga la tatu.

Hadi wanakwenda mapumziko, Simba ilikuwa mbele kwa mabao hayo matatu, kipindi cha pili kilianza kwa kasi lakini vijana wa Gendarmeria walionekana kujilinda zaidi ili wasifungwe magoli mengi.

Emmanuel Okwi aliipatia Simba bao la nne dakika tatu za nyongeza, kwa ushindi huo Simba imejiweka katika mazingira mazuri ya kusonga Raundi ya kwanza na kuna uwezekano wa kukutana na El Masri ya Misri

Emmanuel Okwi akishangilia moja ya mabao aliyofunga

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA