SIMBA WATUA SALAMA SHINYANGA, KUWAVAA MWADUI KESHO
Na Paskal Beatus. Shinyanga
Kikosi cha wachezaji wa Simba Sc wametua salama leo mjini Shinyanga baada ya safari yao waliyoianza alfajili ya leo kwa kutumia usafiri wa ndege.
Simba Sc inayoongoza Ligi Kuu Bara imetua salama na kesho jioni itakuwa mgeni wa timu ya Mwadui Fc katika uwanja wa Mwadui Complex, katika mchezo wa kwanza Simba iliifunga Mwadui mabao 3-0.
Ligi hiyoinaendelea leo kwa mchezo mmoja tu ambapo bingwa mtetezi Yanga Sc itakapowaalika Majimaji Songea katika uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam