SIMBA WASEMA HAWAIOGOPI AL MASRY
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Uongozi, wanachama na wapenzi wa wawawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika, Simba Sc wamesema hawaiogopi wala kuihofia hata kidogo timu ya Al Masry ya Misri ambao ni wapinzani wao katika mchezo ujao.
Akizungumza na mtandao huu, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara, amesema klabu yake haina hofu kabisa na mchezo huo kwani wao hesabu zao ni kusonga mbele.
Manara ameyasema hayo juzi mara baada ya Simba kufanikiwa kuingia raundi ya pili ya kombe la Shirikisho kwa kuitoa mashindanoni timu ya Gendarmarie ya Djibout kwa jumla ya mabao 5-0 baada ya ushindi wa 4-0 nyumbani na 1-0 ugenini.
Simba hawaihofii Al Masry hata kama inatokea Misri ambapo timu zake zimekuwa zikizisumbua timu za Tanzania, lakini Manara akakumbushia pale Simba ilipoitoa nishai Zamalek mwaka 2003 ambapo amedai wembe uleule walioutumia kwa Zamalek watautumia kwa Al Masry