Selembe atimka Majimaji
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Kiungo mshambuliaji Seleman Kassim Selembe inasemekana ametimka katika kikosi cha Majimaji Fc ya Songea na kuonekana visiwani Unguja.
Afisa Habari wa Majimaji, Onesmo Ndunguru amethibitisha kutimka kwa mchezaji huyo ambaye aling' ara katika michuano ya Chalenji iliyofanyika nchini Kenya, Desemba mwaka jana.
Kwa mujibu wa Ndunguru, Selembe bado ana mkataba ba Majimaji hivyo kitendo chake cha kutoroka ni utovu wa nidhamu, lakini awali Selembe aliufuata uongozi wa Majimaji na kuwataka wavunje naye mkataba ili akajiunge na DC Motema Pembw ya DR Congo iliyoonyesha nia ya kumsajili baada ya kuvutiwa naye kwenye Chalenji.
Uongozi wa Majimaji umegoma kumwachilia mchezaji huyo aende bure Motema Pembe na imewataka Wakongoman hao wafanye nao mazungumzo ili wawauzie Selembe, inasemekana Motema Pembe hawako tayari kuvunja mkataba ila wanamtaka Selembe bure