Ruvu Shooting yaiweka "Danger Zone" Kagera Sugar
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Timu ya Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani, jana jioni imeichapa Kagera Sugar mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara katika uwanja wa Mabatini, Mlandizi Kibaha Pwani.
Ushindi huo unaifanya Ruvu Shooting inayonolewa na Abdulmatik Haji kufikisha pointi 17 na kuchupa hadi nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara huku sasa ikiiweka shakani Kagera Sugar ikichungulia tundu la kushuka daraja.
Mabao ya Ruvu Shooting yenye msemaji wake asiyeishiwa maneno, Masau Bwire yalifungwa na Khamis Mcha "Vialii" dakika ya 55 na Alinanuswe Martin dakika ya 79