RAIS WA FIFA AAHIDI NEEMA TANZANIA
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu duniani, (FIFA) Gianny Infatinho amemuahidi Waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa kuwa Shirikisho lake litawekeza nchini.
Bosi huyo wa Fifa ameyasema hayo leo Magogoni Dar es Salaam alipomtembelea waziri mkuu, Infantinho amedai Tanzania ni sehemu nzuri kuwekeza kutokana na amani na utulivu uliopo.
Uongozi wote wa Shirikisho la soka ulimwenguni pamoja na wa mabara yote waliwasili jana nchini kuanza mkutano mkubwa wa Shirikisho hilo ambapo Tanzania inawakilishwa na Rais wa Tff, Wallace Karia, Kaimu katibu mkuu, Wilfred Kidao na mwenyekiti wa BMT, Leodegar Tenga