RAIS MAGUFULI KUMLAKI RAIS WA FIFA
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli anatazamiwa kuupokea ugeni mzito wa Shirikisho la kandanda duniani, (FIFA) unaotarajiwa kuwasili nchini wiki ijayo.
Taarifa iliyotolewa leo na waziri wa habari, michezo, sanaa na utamaduni, Mhe Harrison Mwakyembe inasema kuwa Rais Magufuli ataupokea ugeni huo na kufanya mazungumzo na Rais wa Fifa, Gianni Infantinho.
Mwakyembe leo alikuwa akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari ambapo amedai serikali imeamua kuisaidia TFF katika mapokezi ya viongozi hao wa soka duniani.
Infantinho atapokewa na Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika, (CAF) Ahmad Ahmad, mkutano mkuu wa Fifa utafanyika hapa nchini na kwa mujibu wa Mwakyembe, amedai hata kama Rais Magufuli atashindwa kuhudhuria basi atawakilishwa na makamu wa Rais, Bi Samia Suluhu Hassan au waziri mkuu, Kassim Majaliwa