NYOSO AFUNGIWA MECHI 5 KWA KUMDUNDA SHABIKI
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Beki wa Kagera Sugar "Wana mkurukumbi", Juma Said Nyoso amefungiwa mechi tano pamoja na kupigwa faini ya shilingi Milioni moja kwa kitendo cha kumpiga shabiki wa Simba Sc.
Kamati ya masaa 72 ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini, (TFF) imetoa adhabu hiyo kwa beki huyo mtukutu aliyewahi pia kuzichezea Ashanti United, Simba Sc, Coastal Union na Mbeya City.
Beki huyo alimpiga vibaya shabiki wa Simba Sc katika uwanja wa Kaitaba Bukoba wakati Simba ilipoumana na Kagera Sugar, kamati hiyo imemkuta Nyoso ana hatia ya kumpiga shabiki huyo aliyekuwa akishangilia ushindi wa timu yake ya Simba wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar.
Nyoso alimpiga mateke shabiki huyo anayedaiwa kumpulizia vuvuzela masikioni mwake, awali Nyoso aliwahi kufungiwa miaka miwili baada ya kumtomasa makalioni nahodha wa zamani wa Azam Fc, John Raphael Bocco