Niyonzima aenda India kutibiwa
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Kiungo wa kimataifa wa vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba Sc, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda, amesafiri leo kuelekea nchini India kwa ajili ya matibabu yake ya goti linalomsumbua.
Niyonzima aliyehamia Simba mwanzoni mwa msimu huu akitokea kwa mahasimu wao Yanga Sc, aliweza kuitumikia Simba mwanzoni mwa msimu na kuumia goti lililomtesa kipindi chote mpaka leo kupaa zake kwenda India.
Uongozi wa Simba umehakikisha mchezaji huyo muhimu anatibiwa upesi ili kuungana na wenzake, Said Mohamed Nduda naye alienda kutibiwa India na sasa amerejea uwanjani