Mwadui Fc kuishika sharubu Simba leo

Na Paskal Beatus. Shinyanga

Timu ya Mwadui Fc ya mkoani Shinyanga, jioni ya leo inatelemka uwanja wa CCM Kambarage kuwakaribisha Simba Sc ya Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Mwadui inayomakata nafasi ya 12 ikiwa na pointi 18 itaingia uwanjani kwa lengo la kuishika sharubu Simba hasa ikitaka ushindi ili kuchupa hadi nafasi ya 7, pia wanahitaji kushinda ili kulipiza kisasi baada ya kufungwa katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam.

Kikosi hicho kitaingia uwanjani kikijivunia nyota wake Awesu Awesu, Awadh Juma na Hassan Kabunda kwa vyovyote kinaweza kuibuka na pointi tatu muhimu, lakini Simba nao wanataka kujiimarisha kileleni kwani hadi sasa inaongoza ligi ikiwa na pointi 41 ikifuatiwa kwa karibu na hasimu wake Yanga mwenye pointi 37.

Simba itaingia uwanjani ikitaka kuendeleza wimbi la ushindi ili ijiwekee mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa Bara, Simba itawategemea zaidi nyota wake Emmanuel Okwi raia wa Uganda, Shiza Kichuya na John Bocco "Adebayor"

Mwadui inacheza na Simba leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA