MSUVA APIGA HAT TRICK, CHAMA LAKE LIKIIUA BENFICA 10-0

Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva ameendelea kutakata katika klabu yake mpya ya Difaa El Jadida ya Morocco baada ya usiku wa jana kuifungia mabao matatu katika ushindi wa mabao 10-0 dhidi ya Benfica ya Guinea Bissau, mchezo wa Ligi ya mabingwa barani Afrika uwanja wa Ben Ahmed mjini Jadida, Mazghan, Morocco.

Msuva aliyejiunga na timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu akitokea Yanga Sc ya Tanzania, aliweza kufunga mabao yake hayo katika dakika za 44, 72 na 88.

Mabao mengine ya Difaa El Jadida yamefungwa na Bakary N' diaye aliyefunga matano  dakika za 23, 26, 37, 42 na 47 na lingine likafungwa na Bilal El Magri dakika ya 54

Simon Msuva aliyebebwa, amefunga magoli matatu timu yake ikishinda 10-0

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA