MASIKINI HIMID MAO, KUKAA NJE WIKI SITA
Na Alex Jonathan. Dar es Salaam
Kiungo wa mabingwa wa kombe la Mapinduzi, Azam Fc Himid Mao Mkami atalazimika kukaa nje kwa kipindi cha wiki sita kuuguza majeraha baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini, kiungo huyo alianza kukosekana katika michezo kadhaa ya timu yake ya Azam Fc na kupelekea kuyumba kwa kikosi hicho.
Mao ambaye anafahamika kwa jina la Ninja kutokana na uchezaji wake, aliumia akiwa na kikosi hicho na alishindwa kuendelea kuichezea timu hiyo ambayo imempa majukumu ya unahodha.
Azam Fc mpaka sasa inashikilia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 35 huku ikishuka uwanjani mara 19, kikosi hicho kitaumana na KMC siku ya Jumamosi katika michuano ya Azam Sports Federation Cup hatua ya 16 Bora