Manara awaangukia Yanga

Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Sunday Manara "Computer" ni kama amewaangukia Yanga, baada ya kuwataka wapenzi na mashabiki wa Simba kuacha kuizomea Yanga kesho, itakapocheza na timu ya Saint Louis ya Shelisheli.

Yanga Sc kesho inacheza na Saint Louis ya Shelisheli katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam raundi ya kwanza Ligi ya mabingwa Barani Afrika.

Imekuwa kawaida mashabiki wa Simba au Yanga kushangilia timu za nje zinapokutana na Simba au Yanga, hivyo Manara anawaomba Simba wenzake kuishangilia Yanga kesho ili mashabiki wa Yanga nao wawashangilie Jumapili ya keshokutwa watakapoumana na Gendarmerie ya Djibout zitakapoumana uwanja wa Taifa Dar es Salaam raundi ya kwanza kombe la Shirikisho barani Afrika

Haji Manara amewataka mashabiki wa Simba kushangilia Yanga kesho

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA