MAHADHI AIBEBA YANGA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Na Saida Salum. Dar es Salaam

Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga Sc jioni ya leo imeanza vema kampeni yake ya kusonga mbele katika michuano ya kimataifa, baada ya kuilaza Saint Louis ya Shelisheli bao 1-0 mchezo wa Raundi ya awali, Ligi ya mabingwa barani Afrika, uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo haukuwa rahisi kwa Yanga kama watu walivyodhani kwani ilisubiri hadi kipindi cha pili dakika ya 66 kupata bao la ushindi lililofungwa na kiungo mshambuliaji Juma Mahadhi aliyeunganisha mpira wa kona iliyopigwa na Geofrey Mwashiuya.

Vijana wa Saint Louis waibana vilivyo Yanga na kulifikia mara kwa mara lango isipokuwa umahiri wa kipa wa Yanga, Ramadhan Kabwili kulisaidia kuokoa hatari zote.

Yanga sasa itakuwa na kazi ugenini ya kuzuia isifungwe mabao 2-0 kwani ikikubali kichapo hicho itayaaga mashindano hayo, Obrey Chirwa alikosa penalti kipindi cha kwanza baada ya Hassan Kessy kufanyiwa faulo kwenye eneo la hatari

Juma Mahadhi ameibeba Yanga leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA