LEO NI ZAMU YA WEKUNDU WA MSIMBAZI KIMATAIFA

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Wekundu wa Msimbazi, Simba Sc jioni ya leo inatupa kete yake ya kwanza kimataifa itakapowakaribisha timu ya Gendermarie Tnale ya Djibout mchezo wa Raundi ya awali kombe la Shirikisho barani Afrika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Simba inarejea kwa mara ya kwanza kwenye michuano hiyo baada ya kusota kwa miaka minne kutafuta nafasi ya kushiriki, na kipindi chote imekuwa ikihaha kubadili makocha ili angalau ijipatie tiketi hiyo na mwaka jana Mcameroon Joseph Omog akaiwezesha kutwaa kombe la FA na mwaka huu kurejea kimataifa.

Ikiingia katika mchezo huo, Simba inahitaji ushindi mnono ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele zitakaporudiana juma lijalo, Simba leo itawategemea zaidi nyota wake kama Emmanuel Okwi, John Bocco "Adebayor", Shiza Kichuya, Erasto Nyoni, Asante Kwasi na mlinda mlango wake Aishi Manula.

Wawakilishi wengine wa Tanzania Yanga Sc jana ilipata ushindi kiduchu kwa kuilaza Saint Louis ya Shelisheli bao 1-0 katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ushindi ambao unawaweka shakani.

JKU ya Zanzibar nayo ikalazimishwa sare tasa 0-0 na Zesco ya Zambia mchezo wa Raundi ya awali Ligi ya mabingwa barani Afrika, uwanja wa Amaan, Zanzibar, leo pia Zimamoto inawaalika Dicha ya Ethiopia katika uwanja huo huo wa Amaan, kombe la Shirikisho Raundi ya awali

Simba Sc inacheza na Gendetmarie ya Djibout

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA