LEO NI VITA KALI YA POLISI TANZANIA NA WAKULIMA WA ALIZETI, NAMFUA

Na Ikram Dar es Salaam

Michuano ya Azam Sports Federation Cup leo inaendelea tena kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja tofauti hapa nchini, lakini vita kali itapigwa jioni kule kwenye dimba la Namfua mjini Singida likiwahusisha wenyeji Singida United na Polisi Tanzania.

Hiyo itakuwa moja kati ya mechi kali na ngumu kutokana na ushindani wenyewe wa michuano hiyo iliyofikia hatua ya 16 bora, tayari timu ya Njombe Mji ya mkoani Njombe imeshatangulia robo fainali baada ya kuiondosha Mbao Fc ya Mwanza kwa mikwaju ya penalti 6-5 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.

Lakini pia usiku wa leo katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, kutapigwa mchezo mwingine mkali kati ya vijana wa Manispaa ya Kinondoni, KMC wanaonolewa na beki na kocha wa zamani wa Yanga, Fred Minziro, watakapoumana na Azam Fc.

Michuano hiyo itaendelea tena kesho Jumapili ambapo Majimaji ya Songea itawaalika Yanga katika uwanja wa Majimaji, na Buseresere itawakaribisha Mtibwa Sugar, Jumatatu, Kiluvya United itaikaribisha Mtibwa Sugar uwanja wa Filbert Bayi mjini Kibaha na Stand United itaumana na Dodoma Fc uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga

Singida United wanaumana na Polisi Tanzania leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA