Kagera Sugar yaishika koo Azam

Na Paskal Beatus. Dar es Salaam

Timu ya soka ya Kagera Sugar ya Misenyi mkoani Kagera jioni ya leo imeikaba koo Azam Fc na kwenda nayo sare ya kufungana bao 1-1 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Kwa matokeo hayo Kagera Sugar imepanda kwa nafasi moja kutoka mkiani hadi ya 16 kwa kufikisha pointi 14 na mechi 18 huku Azam Fc ikibaki nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi 34 sawa na Yanga tofauti yao ni magoli ya kufunga na kufungwa.

Timu hizo hadi zinaenda kupumzika dakika 45 zilikuwa hazijafungana, kipindi cha pili Kagera Sugar walitangulia kupata bao la kuongoza lililofungwa na beki Eladslaus Mfulele dakika ya 50 kabla ya Azam Fc kusawazisha kupitia kwa Iddy Kipagwile dakika ya 53

Kagera Sugar wameishika koo Azam Fc leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA