CHIRWA KUSAKA HAT TRICK NYINGINE LEO

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea tena hii leo kwa mchezo mmoja kupigwa jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Uhuru zamani ukijulikana Taifa.

Mabingwa watetezi Yanga Sc watashuka dimbani kuumana na Wandengeleko Majimaji Fc toka Songea mechi ikipigwa jioni ya leo.

Kocha mkuu wa Majimaji, Habib Kondo yeye amejinasibu kupata matokeo katika mchezo huo huku msemaji wa Yanga, Dissmas Ten ametamba kushinda mchezo huo ili waweze kutetea ubingwa wao wa Bara.

Lakini mshambuliaji wa Yanga, Mzambia Obrey Chirwa, anatarajia kuongeza idadi ya mabao ili aweze kutwaa kiatu cha dhahabu, Chirwa ana mabao 10 akiwa nyuma ya Mganda, Emmanuel Okwi mwenye mabao 13.

Chirwa alifunga mabao matatu peke yake katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Njombe Mji ambapo Yanga ilishinda mabao 4-0, hivyo na leo tena Chirwa anatarajia kupiga hat trick nyingine

Obrey Chirwa anasaka hat trick nyingine leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA