AZAM YAJIONDOA MBIO ZA UBINGWA, YABANWA NA LIPULI
Na Mwandishi Wetu. Iringa
Mabingwa wa kombe la Mapinduzi, Azam Fc jioni ya leo imelazimishwa sare tasa 0-0 na wenyeji Lipuli Fc mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uwanja wa Samora mjini Iringa.
Matokeo hayo yanazidi kuwaondoa Azam kwenye mbio ya ubingwa na kuzipisha Simba na Yanga zikichuana kileleni huku pia ikiwapa nafasi Singida United kuwakimbiza.
Azam Fc imefikisha pointi 35 katika michezo 19 waliyocheza, Lipuli nao wanafikisha pointi 20 pia wakicheza mechi 19.