ALIYEVUMA
RAMADHAN LENNY, KIUNGO BORA ALIYEPITA MSIMBAZI.
Na Shafih Matuwa
Jina la Ramadhan Lenny Maufi si geni masikioni mwa wapenzi wa mpira wa miguu hapa nchini hasa wale wa miaka ya 90, kwa vijana wa kileo inawezekana ikawa changamoto kumfahamu.
Na ndio maana Mambo Uwanjani imeamua kuwaletea makala fupi ya kuwakumbusha nyota waliopata kutamba huko nyuma tena wale WALIOVUMA.
Leo hii tumemmulika kiungo fundi kabisa ambaye inasemekana hajawahi kutokea katika kikosi cha Simba kwa misimu yote tangia ilipoanzishwa mwaka 1936, si mwingine ni Ramadhan Lenny Maufi ambaye kwa sasa ni marehemu.
Lenny alikuwa kiungo mkabaji namba sita ambaye hakuna mfano wake tena, hata hao akina Seleman Matola, Jonas Mkude na wengineo hawamfikii.
Lenny amekufa na ubora wake, aliisaidia Simba kutamba katika ngazi mbalimbali za ndani na nje, Simba kuchukua ubingwa wa Bara haikuwa shida kama ilivyo sasa inasotea mwaka wa tano huu haijachukua.
Simba ilikuwa ikitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya muungano wakati huo ilikuwa ikichezwa kwa kushirikisha timu tatu za juu kutoka bara na tatu za juu kutoka visiwani.
Wakati huo wachezaji wa Kitanzania walikuwa na soko katika falme za Kiarabu, hivyo Lenny alikuwa akienda mara kwa mara kucheza soka la kulipwa aidha Oman au Dubai, Waarabu walikuwa wanamkubali sana.
Fundi huyo wa mpira ambaye mdogo wake alikuwa akiichezea Pilsner ya Dar es Salaam, Kaingilila Lenny Maufi, kwa hakika atakumbukwa hasa pale alipoisaidia Simba kutwaa ubingwa wa vilabu Afrika mashariki na kati sasa kombe la Kagame mara mbili mfululizo.
Pia Lenny alikuwemo kwenye kile kikosi kilichoingia fainali ya kombe la CAF mwaka 1993 Simba ilicheza na Stella Abidjan katika uwanja wa Taifa sasa Uhuru na kufungwa mabao 2-0.
Kimetajwa kikosi bora cha Simba cha muda wote kuwahi kutokea, Lenny ameonekana ndiye namba sita bora, ukimtazama huwezi kuamini vitu vyake uwanjani, ana utege flani hivi miguu kutokelezea kwa ndani, duh lakini balaa, akiunasa mpira hatari