YANGA YAMTEMA RASMI ZUTTAH

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, imemuondoa rasmi katika orodha ya usajili beki wake wa kimataifa, Mghana Joseph Zutah.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana jijini jana kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo, zinaeleza kuwa Zutah anatarajiwa kuondoka nchini leo na kurejea kwao Ghana.

Taarifa zaidi kutoka Yanga zinaeleza kuwa licha ya kuwa mchezaji huyo alishalipwa fedha za awali za usajili ambazo ni Dola za Marekani 10,000, kiwango chake hakijawaridhisha viongozi wa klabu hiyo.
"Tayari wameshakubaliana aondoke na kesho (leo), ndiyo anaondoka nchini kurudi kwao," kilieleza chanzo chetu.

Habari zaidi zinaeleza kuwa, Yanga imeamua kuachana na nyota huyo kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake alichoonyesha kwenye michuano ya Kombe la Kagame baada ya kuona hana tofauti na wazawa wengi ambao si wa gharama kama yeye.


Ziliendelea kueleza kuwa, kwa sasa wanatafuta wachezaji wengine watakaoimarisha timu yao kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi ya Bara na mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kuondoka kwa Zutah, kunafanya wachezaji wa kigeni waliobaki Yanga kuwa wanne ambao ni pamoja na Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite kutoka Rwanda, Andrey Coutinho ( Brazil) na Donald Ngoma kutoka Zimbabwe.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA