SHERMAN APIGWA BEI 'SOUTH', MILIONI 300 ZATUA YANGA

MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Mliberia Kpah Sean Sherman amesaini Mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Mpumalanga Black Aces ‘AmaZayoni’ ya Afrika Kusini.

Habari za ndani zinasema Yanga SC italipwa dola za Kimarekani 150,000 (Sh. Milioni 300) kama ada ya uhamisho ya mchezaji huyo aliyesaini Jangwani kwa dola 60,000 (Sh. Milioni 120,000) Desemba mwaka jana.

Na Sherman aliyekuwa analipwa doka 3,000 (Sh. Milioni 6) kwa mwezi Yanga SC, sasa atakuwa analipwa dola 5,000 (Sh, Milioni 10) Black Aces kabla ya kukatwa kodi.

Mwenyekiti wa Aces, Mario Morfou amesema kwa simu leo kwamba wanatarajia Sherman atakuwa pacha mzuri wa Mzambia, Collins Mbesuma katika safu ya ushambuliaji ya timu yake msimu huu.

“Ni mchezaji mzuri na mmoja wa wachezaji bora sana tuliowahi kusaini na sasa tunajivunia kuwa naye AmaZayoni,” amesema Morfou.
Sherman alijiunga na Yanga SCS Desemba mwaka jana akitokea klabu ya Cetinkaya ya Ligi Kuu ya Cyprus Kaskazini na katika kipindi hicho ameichezea timu ya Jangwani mechi 27 na kuifungia mabao sita kwenye mashindano yote.


Mchezaji huyo mwenye umri wa miak 23 sasa, alianza kuichezea Cetinkaya mwaka 2012, akitokea Duzkaya SK aliyoanza kuichezea mwaka
2010, akitokea Barrack YC ya nyumbani kwao, Liberia ambayo alianza kuichezea mwaka 2009.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA