Kolarov, Nasri wasaidia Man City kutua kileleni

Aleksandar Kolarov

Aleksandar Kolarov na Samir Nasri waliwezesha Manchester City kupata ushindi nadra wa 2-0 ugenini Everton Jumapili wakifikia rekodi ya klabu hiyo na kuwafikisha kileleni mwa Ligi ya Premia.

City walikuwa awali wameshinda mechi moja pekee kati ya sita walizochezea Goodison Park – ushindi huo wa pekee ukiwa kwenye safari yao ya kushinda taji 2014.

Kutwaa tena taji hilo ndilo lengo lao msimu huu baada yao kutumia pesa nyingi tena kujengwa upwa kikosi, hesabu ambayo huenda ikaongezeka wakifanikiwa kushawishi Wolfsburg kuwauzia kiungo muhimu Kevin De Bruyne.

Vijana hao wa Manuel Pellegrini wamepata mwanzo bora zaidi kwenye kampeni yao baada ya kuandikisha ushindi mara tisa mfululizo ligini kwa mara ya kwanza tangu 1912 na kufikisha kikomo mwanzo wa kutoshindwa wa Everton msimu huu.


City hawakuweza kumtumia Nicolas Otamendi waliyemnunua £32 milioni kikosini, mlinzi huyo wa zamani wa Valencia akiwa bado hajapokea kibali chake cha kufanyia kazi Uingereza ili kumuwezesha kucheza Ligi ya Premia.

Lakini hata hivyo, mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina anakabiliwa na kubarua kigumu kuengua nahodha Vincent Kompany au Eliaquim Mangala kutoka sehemu ya kati ya ulinzi, wawili hao wakianza tena kikosini kwenye timu ile ile ambayo Pellegrini alitumia kulaza Chelsea 3-0 wiki iliyopita.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA