ARSENAL WAWEKWA KUNDI MOJA NA BAYERN

Olivier Giroud 

Arsenal watakutana na Bayern Munich Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya tatu katika misimu minne baada ya kuwekwa pamoja na klabu hiyo ya Ujerumani hatua ya makundi.

Manchester United watakabiliana na PSV Eindhoven wanaporejea tena dimba hilo kuu la Ulaya, mshambuliaji wao mpya Memphis Depay akilazimika kukabili klabu aliyotoka kabla ya kuhamia Old Trafford.

Chelsea nao watakabiliana na Porto, ambao kocha wao Jose Mourinho aliongoza kushinda dimba hilo 2004.

Manchester City wamepangwa kundi moja na Juventus kutoka Serie A, mabingwa wa Europa League Sevilla na Borussia Monchengladbach ya Ujerumani. Vijana wa Arsene Wenger pia watakutana na Olympiakos ya Ugiriki na Dinamo Zagreb ya Croatia.


Kando na PSV, United watakutana pia na klabu ya CSKA Moscow kutoka Urusi na klabu iliyomaliza ya pili ligi ya Ujerumani Wolfsburg.

Kundi la Mourinho Chelsea linakamilishwa na mabingwa wa Ukraine Dinamo Kiev na Maccabi Tel Aviv ya Israel.

Droo kamili: 

Kundi A: Paris Saint-Germain, Real Madrid, Shakhtar Donetsk, Malmo
Kundi B: PSV, Manchester United, CSKA Moscow, Wolfsburg
Kundi C: Benfica, Atletico Madrid, Galatasaray, Astana
Kundi D: Juventus, Manchester City, Sevilla, Borussia Monchengladbach
Kundi E: Barcelona, Bayer Leverkusen, Roma, BATE Borisov
Kundi F: Bayern Munich, Arsenal, Olympiacos, Dinamo Zagreb
Kundi G: Chelsea, Porto, Dynamo Kiev, Maccabi Tel-Aviv
Kundi H: Zenit St Petersurg, Valencia, Lyon, Gent.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA