WADAU WAMPONDA KOCHA STARS, WADAI BORA YA KIM POULSEN
Wachambuzi wa soka wamesema timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ haina kiwango cha kuvutia uwanjani na imepoteza mvuto.
Wakizungumza baada ya kuishuhudia Taifa Stars ikilazimishwa sare ya bao 1-1 na Malawi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika Mwanza juzi, walisema wanauona mwisho mbaya wa kocha Mholanzi, Mart Nooij.
Kocha Joseph Kanakamfumu aliliambia gazeti hili kuwa Nooij hajaibadilisha Stars na inacheza ili mradi tu tofauti na mtangulizi wake, Kim Poulsen.
Kanakamfumu alisema jambo kubwa analokosea Mholanzi huyo ni uteuzi wa kikosi chake, hasa aina ya wachezaji anaowaita kwani wengi wao hawako fiti.
“Nikiangalia hajaibadilisha timu tofauti na wakati wa Kim kwani timu ilikuwa unaona kabisa inacheza mpira mzuri, lakini kwa huyu timu haichezi kwa mpangilio, hatuoni mtiririko mzuri uwanjani, kila mchezaji anajichezea anavyojua yeye,” alisema Kanakamfumu.
Aliongeza: “Tatizo kubwa anapokosea ni kwenye uteuzi wa timu yake, inatakiwa aangalie wachezaji anaowaita wapo vizuri namna gani kulingana na mfumo anaoutumia, kwani wachezaji wengi aliowaita hawaendani na mfumo wake wa kujilinda.”
Naye Eugine Mwasamaki alisema tatizo liko kwa kocha na hata wachezaji wake kwani kiwango cha timu hiyo si kizuri na kinasikitisha.
Mwasamaki alisema anachoshangaa ni Nooij kuwaita kikosini wachezaji ambao hata kwenye klabu zao hawachezi na kuwacha wengi wanaoonyesha viwango vizuri kwenye mechi Ligi Kuu Bara.
Wachezaji ambao hawana namba ya kudumu katika klabu zao kwa sasa, lakini wapo Stars ni pamoja na Mwadin Ally, Amri Kiemba, Deo Munishi na John Bocco.
“Nashangaa, inawezekana kocha mwenyewe ana matatizo au wanaomsaidia hawana sifa za kumsaidia, kwani kadri muda unavyokwenda kiwango cha timu kinaporomoka. Niseme tangu kuondoka kwa Maximo kwenye timu ya Taifa, hakuna kocha mwingine aliyeleta mabadiliko ndani ya timu hii,” alisema Mwasamaki.